Msaada, Mrejesho na mfumo wa kutoa taarifa za dosari

Unapotuma maombi ya kupata msaada,Mrejesho au kutoa taarifa ya tatizo, tafadhali jumuisha taarifa nyingi kadri uwezavyo:

 1. Operating System unayotumia
 2. Toleo Tor Browser
 3. Kiwango cha ulinzi wa Tor Browser
 4. Hatua kwa hatua namna ya kufikia jambo, ili tuweze kuzalisha tenat (mfano.Nimefungua kivinjali, kwa kuandika url, nikabofya machaguo ya mpangilio, kisha kivinjali changu kikaacha kufanya kazi) 5.Picha ya skrini ya tatizo 6.Zingatia dosari katika Tor Browser ya kompyuta (zinaweza kufunguliwa kwa Ctrl+Shift+J on Windows/Linux and Cmd+Shift+J on macOS)
 5. Dosari za Tor (Settings > Connection > Advanced > View the Tor logs)
 6. Sehemu unayofanya mawasiliano katika Tor. 9.Eneo lililochaguliwa Connection Assist (kama ni matatizo yanayohusiana na Connection Assist )
 7. Je Tor imedhibitiwa katika eneo ulilopo?
 8. Kama Tor imeunganishwa, itachukua muda gani kutafuta data? AAthali yoyote katika kasi ya kuperuzi?

Saa za ofisi za timu ya usaidizi wa watumiaji wa Tor

Jumatatu hadi Alhamisi: njia zetu za usaidizi wa watumiaji kwenye barua pepe, Telegramu, WhatsApp na Signal zinafanya kazi.

Ijumaa hadi Jumapili: nambari ya usaidizi imefungwa. Tafadhali uwe na uhakika timu yetu itarejelea jumbe zako Jumatatu.

Namna ya kutupata

Kuna njia mbalimbali za kuwasiliana nasi,tafadhali chagua ipi itakufaa zaidi.

Telegram

Tuna Telegram bots na njia za mawasiliano rasmi:

 1. @GetTor_Bot ili pakuaTor Browser.
 2. @GetBridgesBot kupata obfs4 bridges.
 3. @TorProject kupata taarifa za toleo jipya.
 4. @TorProjectSupportBot kwa ajili ya msaada.
  • Kwa sasa, Mawasiliano ya Telegram yanapatikana katika njia mbili: Kingereza na Kiurusi.
  • Kama unahitaji msaada katika kukwepa udhibiti wa mtandao, tafadhali chagua katika menyu sehemu unayofanyia mawasilanosababu itakuwa rahisi kwa sisi kufanya ufuatiliaji.

Jukwaa la Tor

Tunashauri kuomba msaada katika Jukwaa laTor. Ili kuwasilisha mada mpya itakubidi utengeneze akaunti. Tafadhali pitia majadiliano yetu ya miongozo kisha angalia mada zilizopo kiabla ya kuuliza. Kwasasa, kwa majibu ya mwisho, tafadhali andika kwa kingereza. Kama utapata tatizo, tafadhali tumia GitLab.

WhatsApp

Unaweza kuwasiliana na nasi kwa kutuma ujumbe wa maandishi katika namba yetu ya WhatsApp: +447421000612. Huduma hii inapatikana tu kwa ujumbe wa mandishi; video au simu hazijawezeshwa.

Signal

Unaweza kupata msaada kwa kutuma ujumbe wa maandishi katika namba yetu ya Signal: +17787431312. Signalni programu ya matumizi ya bure na imelenga ufaaragha kwa watumiaji. kwasasa, mfumo wetu wa msaada unapatikana kwa lugha ya kingereza na kiurusi katika kusaidia watumiaji wa Tor kwa maeneo yaliyodhibitiwa. Huduma hii hupatikana kwa ujumbe mfupi wa maneno tu; video, au simu hazijawezeshwa. Baada ya kutuma ujumbe,watu wetu wa msaada watakusaidia kutatua tatizo.

Barua pepe

Tutumie barua pepe kupitia frontdesk@torproject.org

Katika kichwa cha habari cha barua pepe yako, tafadhali tujulishe unatoa taarifa ya kitu gani. Namna ambavyo kichwa cha habari cha barua pepe kinakuwa mahususi mfano. "Kushindwa kuunganishwa", "mrejesho katika tovuti", "Mrejesho katika Tor Browser, "Nahitaji bridge"), ndivyo itakavyokuwa rahisi kwetu kuelewa na kufuatilia. Wakati mwingine tunapopokea barua pepe zisizo na kichwa cha habari,huingia katika barua pepe zisizothibitishwa na tunashindwa kuziona.

Kwa mrejesho wa mwisho, tafadhali andika katika lugha za kingereza, kiurusi, kihispaniola, kihindi kibangaladeshi//au kireno kama unaweza. Kama hakuna lugha unayoielewa kati ya hizi, tafadhali andika kwa lugha yoyote unayoweza, lakini jua kwamba muda kidogo kujibu sababu tutahitaji msaada wa kutafsiriwa ili kuelewa.

IRC na Matrix

Unaweza kutupata katika #tornjia ya OFTC au chaneli ya kutoa msaada kwa watumiaji wa Tor katika Matrix. Tunaweza tusijibu papo kwa hapo, lakini tunaangalia matatizo yaliyopita na tutakurudia tunapoweza.

Jifunze namna ya kujiunganisha katika IRC / Matrix.

GitLab

Kwanza, angalia kama tatizo limejulikana. Unaweza kutafuta na kusoma matatizo katika https://gitlab.torproject.org/. Kuunda jambo jipya, tafadhaliomba akaunti mpya kuipata Tor Project's GitLab haraka na tafuta hifadhi sahihi kutoa taarifa ya tatizo. Tunafuatilia matatizo yote yahusianayo na Tor Browser Tor Browser issue tracker. Matatizo yahusianayo na tovuti yetu yanatakiwa kujazwa katika Kinasa matatizo ya tovuti.