Tor Browser ni lazima isasishwe wakati wote. Kama unaendelea kutumia toleo lililopitwa na wakati la programu, unaweza kuwa katika hatari ya kupata tatizo kubwa la kiusalama ambazo zitasumbua faragha na kutojulikana kwako.

Tor Browser itakusisitiza kusasisha programu pale tu toleo jipya litakapo toka:menyu kuu (≡)itaonyesha duara la kijani ikiwa na mshale ulioangalia juu, na unaweza kuona kiashiria cha kusasisha kila ukifungua Tor Browser. Unaweza kusasisha mojakwamoja katika mfumo au wewe mwenyewe.

KUSASISHA TOR KIVINJARI KIAUTOMATIKI

Chagua'Restart to update Tor Browser' chini ya menyu kuu

Unaposisitizwa kusasisha Kivinjari cha Tor, bofya katika menyu kuu (≡), Kisha chagua "Update available - restart now".

Boresha sehemu inayoonyesha maendeleo

Subiria maboresho kisha pakua na sakinisha, kisha Tor Browser itaanza yenyewe. Sasa utakuwa unatumia toleo jipya.

KUSASISHA TOR KIVINJARI KWA MUONGOZO

Unaposisitizwa kusasisha Tor Browser, maliza shughuli ya kuperuzi kisha funga programu.

Ondoa Tor Browser katika mfumo wako kwa kulifuta folda lililomo (angalia sehemu ya kuondoa usanikishajifokwa taarifa zaidi).

Tembelea https://www.torproject.org/download/ na upakue nakala ya toleo jipya la Tor Browser lililotolewa, kisha sakinisha kama mwanzo.