JAVASCRIPT

JavaScript ni lugha ya programu ambayo tovuti hutumia kutoa vitu vya kimawasiliano kama vile, video fupi, sauti, na thali katika muda. Bahati mbaya, JavaScript pia inaweza kuruhusu kuvamiwa katika ulinzi wa kivinjari, ambayo hupelekea hali isiyo ya kawaida.

Tor Browser inavitu vya ziada viitwavyo NoScript. Hupatikana kupitia "Preferences" (au"Options" katika Windows) ya hamburger menu (≡), kisha chagua 'Customize' kisha vuta alama ya “S” iliyopo juu kulia katika window. NoScript inakuruhusu kudhibiti JavaScript (na aina zingine za scripts) zilizopo katika tovuti binafsi, au bhuzuia kabisa.

Watumiaji wanahitaji kiwango kikubwa cha ulinzi katika kuperuzi katika mitandao wanatakiwa kuweka Tor Browser’s Kiwango cha ulinzi)katika Safer” (ambayo huzuia JavaScript katika tovuti zisizo na HTTPS ) au “Safest” (ambazo hufanya hivyo kwa tovuti zote). Hatahivyo, kuizuia JavaScript itazuia tovuti nyingi kuonyehs kwa usahihi, hivyo mpangilio wa mojakwamoja wa Tor Browser ni kuruhusu tovuti kutumia scripts katika mfumo wa "Standard".

KIVINJARI NYONGEZA

Tor Browserinapatikana katika Firefox, na inaweza kuongezwa katika kivinjari kingine chochote au maudhui yanayoendana na Firefox yanaweza kusakiniwa katika Tor Browser.

Hatahivyo, vitu pekee vilivyoongezwa ambavyo vimejaribiwa kwa matumizi na Tor Browser ni vile vilivyojumuishwa mojakwamoja. kusanikisha kivinjari kingine chochote inaweza kuzuia utendaji kazi wa in Tor Browser au kusababisha matatizo makubwa zaidi ambayo yanaathili usalama na faragha yako. Haishauriwi kabisa kuongeza vitu vingine, na Tor Project haitatoa msaada kwa usanidi huo.

FLASH PLAYER

Flash ilikuwa programu ya medianuwai iliyotumiwa na tovuti kuonyesha video na vipengele vingine shirikishi kama vile michezo. Ilizimwa kwa chaguomsingi katika Kivinjari cha Tor kwa sababu inaweza kuwa imefichua eneo lako halisi na anwani ya IP. Kivinjari cha Tor hakitumii Flash tena na hakiwezi kuwezeshwa.

Utendakazi mwingi wa Flash umebadilishwa na kiwango cha HTML5, ambacho kinategemea sana JavaScript. Majukwaa ya video kama vile YouTube na Vimeo yamebadilika hadi HTML5 na hayatumii tena Flash.