Unatakiwa kuanza kuperuzi tovuti kwa kutumia Tor Browser smuda mfupi baada ya kutumia programu, na bofya kitufe cha “Connect” kama unatumia kwa mara ya kwanza.

Bofya'Connect' kuunganishwa na Tor

Connection Assist hukutaarifu juu ya hali ya uunganishwaji katika mtandao wako kama uta bofya katika 'Test'.

Kipimo cha Connection Assist

Angalia Muunganisho wako wa intaneti ikiwa inasema 'Offline'. Ikiwa muunganisho wako kwenye Mtandao wa Tor haujaanzishwa na inasomeka 'Not Connected' hatua zifuatazo zinaweza kusaidia.

Connection Assist dosari za kutokuwa hewani

UTATUZI WA HARAKA

Kama Tor Browser haiunganishwi, kunaweza kuwa na sukuhusho rahisi. Jaribu kila kimoja katika vifuatavyo:

  • Mfumo wa saa ya kompyuta yako unatakiwa kuwa sahihi, au Tor itashindwa kuunganishwa.
  • Hakikisha Tor Browser nyingine au mfano wa 'Tor'haupo katika mfumo wako. Kama hauna uhakika kama Tor Browser inafanya kazi, anza upya kompyuta yako.
  • Hakikisha programu yoyote ya kuzuia virusi uliyosanikisha haizuii Tor kufanya kazi. Unaweza hitaji kufuatilia taarifa za programu ya kupinga virusi kama hujui namna ya kufanya.
  • Kwa muda mfupi izime program inayochuja usafirishwaji wa data.
  • Kama Tor Browser ilikuwa inafanya kazi awali lakini sasa haifanyi kazi mfumo wako unaweza kuwa umezima kwa muda. Kuzima na kuwasha kompyuta yako kwa kuipumzisha itatatua tatizo.
  • Futa Tor Browserna usakini upya. Kama una sasisha, usiandike tu mafaili yaliyopita ya Tor Browser; hakikisha yamefutwa yote kabla.

MATATIZO MAPYA YA TOR

Mara nyingi, ili kuangalia matatizo ya Torinaweza kusaidia katika kuchunguza tatizo. Kama unapata changamoto katika kuunganisha, ujumbe wa dosari unaweza kutokea na unaweza kiuchagua "copy Tor log to clipboard". Kisha nakili matatizo ya Tor log katika faili la kipimo au nyaraka nyingine.

Kama huoni chaguo hilo na Tor Browser imefunguliwa,Unaweza kutafuta katika menyu iliyofichwa ("≡"),kisha bofya katika "Settings", na mwishoni katika "Connection" sehemu ya machaguor. Chini katika kurasa, pembeni ya maandishi ya "View the Tor logs", bofya kitufe cha "View Logs...".

Njia mbadala, katika GNU/Linux, kuona tatizo hapohapo katika kifaa, peruzi katika saraka ya Tor Browserna ianzishe kutumia Tor Browser kutoka katika sehemu ya amri:

./start-tor-browser.desktop --verbose

Ili kuhifadhi tatizo katika faili (default: tor-browser.log):

./start-tor-browser.desktop --log [file]

Taarifa zaidi kuhusiana na hii zinaweza kupatikana katika Support Portal.

IJE MAWASILIANO YAKO YAMEDHIBITIWA?

Kama bado huwezi kuunganisha na,Mtoa huduma wako wa mtandao anaweza kuwa amezibiti mawasiliano katika Tor network. Soma sehemu yaKukwepa udhibiti kwa ajili ya masuluhisho yanayowezekana.

MASUALA YANAYOJULIKANA

Tor Browser inaendelea kuboreshwa, na kuna baadhi ya matatizo yanajulikana lakini bado hayaja tatuliwa. Tafadhalki angalia kurasa ya Matatizo yanayojulikana kuona kama tatizo unalopitia limeorodheshwa.