Kwa Windows

1.Peruzi katika Tor Browser kurasa ya kupakua.

  1. Pakua faili la .exeWindows .

  2. (Inashauriwa) Hakikisaini ya faili.

  3. Upakuaji ukikamilika, bofya mara mbili kitufe cha faili la .exe. Kamilisha zoezi la kuweka programu ili uweze kutumia.

Kwa macOS

1.Peruzi katika Tor Browser kurasa ya kupakua.

  1. Pakua faili la macOS .dmg .

  2. (Inashauriwa) Hakikisaini ya faili.

  3. Upakuaji ukikamilika, bofya mara mbili kitufe cha file la .dmg. kamilisha zoezi la kuweka program ili uweze kutumia.

Kwa GNU/Linux

1.Peruzi katika Tor Browser kurasa ya kupakua.

Pakua faili la GNU/Linux .tar.xz .

  1. (Inashauriwa) Hakikisaini ya faili.

  2. Sasa fuata njia ya picha au ya amri za maelezo:

Njia ya picha

  • Ukimaliza kupakua, chuja mafaili yaliyohifadhuwa.

  • utaitaji kuiambia GNU/Linux kuwa unahitaji uwezo wa kumia maneno yenye amri . Peruzi katika saraka ya Tor Browser. Bofya kulia katika start-tor-browser.desktop, fungua Properties au Preferences na badilisha ruhusa ya kuruhusu faili lenye maandishi ya amri kuwa kama programu. Bofya mara mbili kitufe cha Tor Browser ili kuanza kutumia kwa mara ya kwanza.

Weka mafile yaliyopo ukurasa wa mbele wa kompyuta katika anwani za vyanzo vya wazi

Zingatia Katika Obuntu na baadhi ya vyanzo vingine vya wazi kama ukijaribu kufungua start-tor-browser.desktop faili lenye maneno linaweza kufunguka. Katika hali hiyo, itabidi ubadilishe tabia chaguo-msingi na kuruhusu faili za running.desktop kama vitekelezo. Mpangilio huu unaweza kupatikana katika kidhibiti chako cha faili.

Njia ya maneno ya maelezo au amri

  • ukimaliza kupakua chuja mafaili yaliyohifadhiwa kwa amri tar -xf [TB archive].

  • Kutoka ndani ya saraka ya Tor Browser, unaweza kufungua Tor Browser:

    ./start-tor-browser.desktop

    Zingatiakama amri hizi zitashindwa kufanya kazi, pengine utahitajika kutengeneza faili lenye amri. Ambayo inataokana na utendaji wa saraka chmod +x start-tor-browser.desktop

Baadhi ya ishara zinazoweka kutumika na start-tor-browser.desktopkutoka katika orodha ya maelezo ya amri:

Flag Maelekezo
--register-app Kusajili Tor Browser kama program ya kompyuta.
--verbose Kuonyesha matokeo ya Tor na Firefox katika kifaa unachotumia.
--log [file] Kuchukua taarifa za matokeo ya Tor na Firefox katika faili (default: tor-browser.log).
--detach Kutoka katika muunganiko na kutumia Tor Browser pembeni.
--unregister-app Kuondoa usajili wa Tor Browser kama programnu ya komyuta.

Angalia hapa namna ya kuhuwisha Tor Browser.