Upatikanaji wa mojakwamoja wa mtandao wa Tor wakati mwingine unaweza kuzuiliwa na mtoa huduma wako wa mtandao au serikali. Tor Browser inajumuisha baadhi ya vifaa vya kukwepa uzuiliwaji wa mtandao kwa kuweza kuwepa uzuiliwaji huo. Vifaa hivi vinaitwa “pluggable transports”.

AINA ZA PLUGGABLE TRANSPORT

Kwa sasa kuna pluggable transports nne zinazopatikana, ila nyingine nyini zinatengenezwa.

obfs4 obfs4 hufanya usafirishaji wa Tor kuwa hauna mpangilio, na pia huzuia wazibiti kupata bridges kwa kuchunguza mtandao, obfs4 bridges zinauwezekano mdogo sana kuzuiliwa kuliko vitangulizi, obfs3 bridges.
meek Usafirishaji wa meek huwa kama unaperuzi tovuti kubwa badala ya kutumia Tor, meek-azur hufanya kuwa kama unatumia tovuti ya Microsoft.
Snowflake Snowflake huelekeza muunganisho wako kupitia seva mbadala zinazoendeshwa na watu waliojitolea ili kuifanya ionekane kama unapiga simu ya video badala ya kutumia Tor.
WebTunnel WebTunnel hufunika muunganisho wako wa Tor na kuifanya ionekane kana kwamba unafikia tovuti kupitia HTTPS.

KUTUMIA USAFIRISHAJI UNAOWEZA KUZIBA

Kutumia pluggable transport, bofya "Configure Connection" unapoanza kutumia Tor Browser kwa mara ya kwanza. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Kutoka katika menu, chagua pluggable transport ambayo ungependa kuitumia.

Pale unapokuwa umechagua pluggable transport, bofya "Connect" kuhifadhi mpangilio.

Au, kama Tor Browser inatumika, bofya "Settings" katika machaguo (≡)na kisha katika "Connection" katika mstari wa pembeni. Chini ya sehemu ya "Bridges", onyesha chaguo la "Choose from one of Tor Browser's built-in bridges" na bofya katika chaguo la "Select a Built-In Bridge". Chagua pluggable transport yoyote unayopenda kutumia toka katika orodha na ubofye "OK". Mpangilio wako kiautomatiki utahifadhiwa mara utapofunga tabo.

Tengeneza built-in bridges

USAFIRI UPI NAWEZA KUTUMIA?

Kila moja katika usafirishaji ulio orodheshwa katika munu ya Tor Bridge huwafanya kazi katika njia tofauti, na ufanisi wake hutegemea mazingina ya mtu binafsi.

Kama unajaribu kukwepa uzuiliwaji wa mawasiliano kwa mara ya kwanza, unatakiwa kujaribu namna nyingine ya usafirishaji :obfs4, snowflake au meek-azure.

Kama unajaribu njia zote hizo, na hakuna inayokuwezesha kupata mtandao, utahitajika kuomba bridge au ingiza anwani ya bridge kawaida.

Watumiaji nchini China watatakiwa kujiunga na obfs4 bridge binafsi ambazo hazijaorodheshwa. Wasiliana nasi kupita Telegram Bot @GetBridgesBot and type /bridges. Au tuma barua pepe kwendafrontdesk@torproject.org ikiwa na maneno "private bridge cn" katika kichwa cha habari. kiwa unaunganisha kutoka nchi nyingine, tafadhali kumbuka kujumuisha nchi aunambari ya nchi yako katika mada ya barua pepe.

Soma sehemu ya Bridgeskujua bridge ni nini na namna ya kuzipata.