Pluggable Transports nyingi, kama vile obfs4, zinategemea matumizi ya "bridge" relays. Kama ilivyo Tor relays za kawaida, madaraja yanaendeshwa na wanaojitolea; tofauti na relays za kawaida,zenyewe hazijaorodheshwa wazi, ili mtu asiye na nia njema akazitambua kwa urahisi.

Kutumia Bridges pamoja na pluggable transports husaidia kuondoa ukweli kwamba unatumia Tor, ila inaweza kupunguza kasi ya mawasiliano ukilinganisha na unapotumia Tor relays za kawaida.

Pluggable transports nyingine, kama vile meek na Snowflake, hutumia mbinu tofauti ya kuzuia udhibiti wa mtandao ambao hautegemei kupatikana kwa anwani ya kiungo. Huhitaji kupata anwani za kiungo ili kutumia usafiri huu.

KUPATA ANWANI ZA BRIDGE

Kwasababu anwani za bridge sio za umma, unatatakiwa kuomba wewe mwenyewe. una machaguzi machache:

  • Tembelea https://bridges.torproject.org/na fuata maelekezo yafuatayo, au
  • Barua pepe bridges@torproject.org kutoka Gmail, au anwani ya barua pepe ya Riseup
  • Tumia Moat kupata madaraja katika Tor Browser.
  • tuma ujumbe kwa @GetBridgesBot katika Telegram. Bonyeza 'Kuanza' au andika /startor/bridgeskatika mawasiliano ya ujumbe. Nakili anwani ya bridge na endelea:
    • Tor Browser ya Kompyuta ya mezani: Bofya katika "mpangilio" katika machaguo ya (≡)na katika "mawasiliano"upande wa pembeni. Katika upande wa "Bridges", kutoka katika machaguo "Ingiza anwani ya bridge ambayo tayari unaifahamu" bofya katika "Ongeza Bridge kwa kawaida"na ingiza kila anwani ya bridge katika mstari tofauti.
    • Tor Browser ya Android: Gusa katika 'Settings' (⚙️) kisha katika 'Config Bridge'. Toggle on 'Use a Bridge' na chagua 'Provide a Bridge I know'. Ingiza anwani ya Bridge.

KUTUMIA MOAT

Kama unaanza kutumia Tor Browser kwa mara ya kwanza, bofya katika "sanidi muungamisho"kufungua ukurasa wa mpangilio wa Tor. Chini ya eneo la "Bridge"onyesha "Request a bridge from torproject.org" kisha bofya "Request a Bridge..." ili BridgeDB ikupatie bridge. Kamilisha Captcha kisha na bofya "Submit". Bofya "Connect"kuweka mipangilio yako.

Au, kama Tor Browser inatumika, bofya "Settings" katika machaguo (≡)na kisha katika "Connection" katika mstari wa pembeni. Katika sehemu ya "Bridges", tafuta "Request a bridge from torproject.org" and click on "Request a Bridge..."ili ridgeDB ikupatie bridge. Kamilisha Captcha kisha na bofya "Submit". Mpangilio wako kiautomatiki utahifadhiwa mara utapofunga tabo.

Omba bridge kutoka torproject.org

INGIZA ANWANI ZA BRIDGE

Kama unaanza kutumia Tor Browser kwa mara ya kwanza, bofya katika "sanidi muungamisho"kufungua ukurasa wa mpangilio wa Tor. Chini ya eneo la "Bridge", kutoka katika machaguo "Ingiza anwani ya bridge ambayo unaijua tayari" bofya katika Bridge" na ingiza kila anwani ya bridge katika mstari tofauti. Bofya "Connect"kuweka mipangilio yako.

Au, kama Tor Browser inatumika, bofya "Settings" katika machaguo (≡)na kisha katika "Connection" katika mstari wa pembeni. Chini ya eneo la "Bridge", kutoka katika machaguo "Ingiza anwani ya bridge ambayo unaijua tayari" bofya katika Bridge" na ingiza kila anwani ya bridge katika mstari tofauti. Mpangilio wako kiautomatiki utahifadhiwa mara utapofunga tabo.

Ingiza anwani ya bridge kawaida

Kama mawasiliano hayatafanikiwa, daraja ulilopokea linaweza kuwa na kasi ndogo. Tafadhali tumia moja kati ya njia hapo juu kupata anwani za bridge nyingi zaidi, na jaribu tena.

BRIDGE-MOJI

Kila anwani ya bridge inawakilishwa na mfuatano wa herufi na tarakimu zinazoitwa Bridge-mojis. Bridge-mojis zinaweza kutumika kuhakiki kuwa bridge iliyokusudiwa imewekwa kwa usahihi.

Bridge-mojis ni vitambulisho vya bridge vinavyoweza kusomeka na binadamu na hufanyasiyohuwakilisha ubora wa mawasiliano katika mtandao wa Tor au hali ya bridge. Mfululizo wa alama haziwezi kutumika kama mahitaji. Watumiaji wanahitaji kutoa anwani ya bridge iliyokamilika ili waweze kuunganishwa na bridge.

Bridge-moji

Anwani ya bridge inaweza kusambazwa kwa kutumia QR code au kwa kuandika anwani husika.

Kanuni ya QR Bridge