Kwa Windows
1.Peruzi katika Tor Browser kurasa ya kupakua.
Pakua faili la .exe
Windows .
(Inashauriwa) Hakikisaini ya faili.
Upakuaji ukikamilika, bofya mara mbili kitufe cha faili la .exe
. Kamilisha zoezi la kuweka programu ili uweze kutumia.
Kwa macOS
1.Peruzi katika Tor Browser kurasa ya kupakua.
Pakua faili la macOS .dmg
.
(Inashauriwa) Hakikisaini ya faili.
Upakuaji ukikamilika, bofya mara mbili kitufe cha file la .dmg
. kamilisha zoezi la kuweka program ili uweze kutumia.
Kwa GNU/Linux
1.Peruzi katika Tor Browser kurasa ya kupakua.
Pakua faili la GNU/Linux .tar.xz
.
(Inashauriwa) Hakikisaini ya faili.
Sasa fuata njia ya picha au ya amri za maelezo:
Njia ya picha
Ukimaliza kupakua, chuja mafaili yaliyohifadhuwa.
utaitaji kuiambia GNU/Linux kuwa unahitaji uwezo wa kumia maneno yenye amri .
Peruzi katika saraka ya Tor Browser.
Bofya kulia katika start-tor-browser.desktop
, fungua Properties au Preferences na badilisha ruhusa ya kuruhusu faili lenye maandishi ya amri kuwa kama programu.
Bofya mara mbili kitufe cha Tor Browser ili kuanza kutumia kwa mara ya kwanza.

Zingatia Katika Obuntu na baadhi ya vyanzo vingine vya wazi kama ukijaribu kufungua start-tor-browser.desktop
faili lenye maneno linaweza kufunguka.
Kubadili tabia hii na badala yake kufungua Tor Browser, fuata hii:
- Fungua "mafaili" (GNOME Files/Nautilus)
- Bofya katika mapendeleo.
- Peruzi katika ukuras wa tabia.
- Chagua "Run them" au "ask what to do" chini ya "Executable Text Files".
- Kama umechagua ifuatayo bofya katika 'Run" baada ya kufungua faili la
start-tor-browser.desktop
.

Njia ya maneno ya maelezo au amri
ukimaliza kupakua chuja mafaili yaliyohifadhiwa kwa amri tar -xf [TB archive]
.
Kutoka ndani ya saraka ya Tor Browser, unaweza kufungua Tor Browser:
./start-tor-browser.desktop
Zingatiakama amri hizi zitashindwa kufanya kazi, pengine utahitajika kutengeneza faili lenye amri. Ambayo inataokana na utendaji wa saraka chmod +x start-tor-browser.desktop
Baadhi ya ishara zinazoweka kutumika na start-tor-browser.desktop
kutoka katika orodha ya maelezo ya amri:
Flag |
Maelekezo |
--register-app |
Kusajili Tor Browser kama program ya kompyuta. |
--verbose |
Kuonyesha matokeo ya Tor na Firefox katika kifaa unachotumia. |
--log [file] |
Kuchukua taarifa za matokeo ya Tor na Firefox katika faili (default: tor-browser.log). |
--detach |
Kutoka katika muunganiko na kutumia Tor Browser pembeni. |
--unregister-app |
Kuondoa usajili wa Tor Browser kama programnu ya komyuta. |
Angalia hapa namna ya kuhuwisha Tor Browser.