( Mara ya kwanza) huduma za Onion zilifahamika kama "huduma zilizofichwa") ni huduma, kama tovuti, ambazo hupatikana tu kupitia Tor network.

Onion services hutoa manufaa kadhaa zaidi ya huduma za kawaida za tovuti zisizo binafsi:

  • Sehemu zinapokaa na anwani ya IP ya Onion services’zimefichwa, kuweka ugumu kwa wapinzani kudhibiti na kutambua shuguli zake.
  • Usafirishaji wote wa data kati ya watumiaji wa Tor na onion services umesimbwa, hivyo huitaji kuhofia kuhusiana na kuunganisha kwa kutumia HTTPS.
  • Anwani ya huduma ya onion hutengenezwa kiotomatiki hivyo waendeshaji hawahitajiki kununua jina la uwanja.
  • Kwa sababu ya usimbaji fiche unaohusika, URL ya .onion huruhusu Tor kuhakikisha kwamba inaunganishwa kwenye eneo linalofaa na kwamba muunganisho hauchezi.

NAMNA YA SASA KUPATA ONION SERVICE

Kama ilivyo katika tovuti nyingine, utahitaji kujua anwani ya huduma ya onion ili kuweza kuunganishwa nazo. Anwani ya onion inajumuisha alama 56 ikifutiwa na ".onion".

Unapotumia tovuti inayotumia onion service, Tor Browseritaonyesha katika sehemu ya kuandika URL alama ya onion itaonyesha hali ya mawasiliano yako: salama na kutumia onion service. Unaweza kujifunza zaidi kuhusiana na huduma za onion ambayo unatembelea kwa kuangalia katika sehemu inayoonyesha Circuit.

Njia nyingine ya kujua tovuti ya onion kama msimamizi wa tovuti haiweka tabia ya Onion-Location. Onion-Location ni taarifa ya HTTP isiyo na viwangoambayo tovuti inaweza kutumia kutangaza onion zingine. Kama tovuti unayotembelea ina onion, ujumbe wa zambarau katika sehemu ya URLkatika Tor Browser utatokea ukionyesha "uwepo wa .onion". Ukibofya katika ".onion available",tovuti itatafuta data tena na kukupeleka katika onion zingine.

Onion-Location

UTHIBITISHO WA ONION SERVICE

Uthibitisho wa onion service ni huduma ambayo tovuti ya onion ambayo inahitaji mtumiaji atoe namba za uthibitisho kabla ya kupata huduma. Kama mtumiaji wa Tor, unaweza kujithibitisha wewe mwenyewe mojakwamoja kwenye Kivinjari cha Tor. Ili kupata huduma hii, utahitaji kupata utambulisho toka kwa mto huduma wa onion service. Unapotumia onion service zilizothibitishwa, Tor Browseritaonyesha katika sehemu ya URL alama ndogo ya kijivu, ikiwa na ujumbe wa maelezo. Ingiza alama zako za utambuzi halisi katika sehemu ya kujaza.

Client Authorization

DOSARI ZA ONION SERVICE

Kama huwezi kujiunga katika tovuti ya onion, Tor Browser wataleta ujumbe maalumu wa uwepo wa dosari kutoa taarifa kwanini tovuti haipatikani. Dosari zinaweza kutokea katika matabaka mbalimbali: dosari za mtumiaji, dosari za mtandao au dosari za huduma. Baadhi ya hizi dosari zinaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kwenda sehemu ya Troubleshooting . Jedwali lifuatalo linaonyesaha dosari zozote zinazoweza kujitokeza na hatua za kuchukua ili kutatua.

Msimbo Jina la Dosari maelezo kidogo
0xF0 Tovuti ya onion Haipatikani Sababu kuu inaweza kuwa tovuti ya onion haipo hewani. Wasiliana na msimamizi wa tovuti ya onion.
0xF1 Tovuti ya Onion Haiwezi kupatikana Tovuti ya onion haipatikani kutokana na dosari za mtandao.
0xF2 Tovuti ya onion haijaonganishwa Sababu kubwa inaweza kuwa tovuti ya onion haiko hewani. Wasiliana na msimamizi wa tovuti ya onion.
0xF3 Haiwezi kuunganishwa na tovuti ya onion Tovuti ya onion inatumika au mtandao wa Tor umezidiwa. Jaribu tena baadaer.
0xF4 Tovuti ya onion inahitaji uthibitisho Ili kuifikia tovuti ya onion kulihitaji alama za utambulkisho na hazikutolewa.
0xF5 Uthibitisho wa tovuti ya onion haujafanikiwa Alama za utambulisho zilizotolewa si sahihi zimekataliwa. Wasiliana na msimamizi wa tovuti ya onion.
0xF6 Anwani ya tovuti ya onion sio sahihi Anwani ya tovuti ya onion sio sahihi. Tafadhali hakikisha umeingiza kwa usahihi.
0xF7 Muda wa kutengeneza Circuit ya tovuti ya onion umeisha Imeshindwa kuunganisha katika tovuti ya onion, inawezekana kutokana na mtandao kuwa dhaifu.

TROUBLESHOOTING

Kma huwezi kupata onion service ulizoomba, hakikisha umeingiza anwani ya onion kwa usahihi; sababu hata kosa dogo tu itaizuiaa Tor Browser kuipata tovuti hiyo.

Ikiwa unajaribu kufikia herufi 16 (huduma fupi ya onion ya "V2"), anwani ya aina hii haifanyi kazi tena kwenye mtandao wa leo wa Tor.

Unaweza pia kujaribu kama unauwezo wa kupata onion services nyingine bkwa kuunganisha katika DuckDuckGo's Onion Service.

Kama bado unashindwa kujiunga katika onion service baada ya kuthibitisha anwani, tafadhali jaribu tena baadae Kunaweza kuwa na matatizo ya muda katika mtandao, au waendeshaji wa tovuti wanaweza kuiruhusu kutokuwa hewani bila kutoa tahadhali.