Njia salama na rahisi ya kupakua Tor Browser ni kutoka katika tovuti rasmi ya Tor Project katika https://www.torproject.org/download. Mawasiliano yako katika tovuti yatakuwa salama kwa kutumia HTTPS,ambayo huleta ugumu zaidi kwa mtu kucheza nayo.

Hatahivyo, kuna wakati ambapo huwezi kuipata tocuti ya Tor Project kwa mfano, kama itakuwa imezuiliwa katika mtandao wako. Kama hii ikitokea, unaweza kutumia moja ya njia za kupakua zifuatazo za mbadala:

NAKALA

Kama unashindwa kupakua Tor Browser kutoka katika tovuti rasmi ya Tor Project, badala yake unaweza kuipakua kutoka katika moja ya nakala zetu rasmi, inaweza kuwa kwa kupitia EFF or Calyx Institute.

GetTor

GetTor ni huduma ambayo mojakwamoja hujibu ujumbe wenye anwani za toleo jipya la Tor Browser, lililopo sehemu mbalimbali, kama vile Dropbox, Google Drive and GitHub.

KUTUMIA GETTOR KUPITIA BARUA PEPE

Tuma barua pepe kwenda gettor@torproject.org,na katika ujumbe kwa ufupi andika “windows”, “osx”, au(((“linux”,(bila alama za funga na fungua semi) kufuatana na mfumo wako wa uchakataji. Kwa mfano ili kupata anwani za kupakua Tor Browser kwa ajili ya Windows, tuma barua pepe kwenda gettor@torproject.org l ikiwa na neno "windows" katika kichwa cha habari.

GetTor itaoa majibu yakiwa na barua pepe yenye anwani ambayo unaweza kupakua Tor Browser, saini ya kriptografia (inahitajika ili kuhakiki upakuliwaji), alama za kipekee za funguo hutumika kutengeneza saini, na vifurushi checksum. Unaweza kupewa chaguo la programu yenye ukubwa wa “32-bit” or “64-bit” kulingana na aina ya kumpyuta unayotumia.

KUTUMIA GETTOR KUPITIA TELEGRAM

Tuma ujumbe kwenda @GetTor_Bot kupitia Telegram.

  • Bofya 'Start' au write /start katika mawasiliano.

  • Chagua lugha yako.

  • Kuna machaguo mawili ya kupakuaT or Browser.

    • Bofya'Send me Tor Browser'na chagua mfumo wako wa kuchakata. GetTor zitajibu zikiwa na mafile ya Tor Browser yanayoweza kupakuliwa na saini zinazoweza kuthibitisha kupakuliwa.
    • Bofya katika 'Send me other mirrors for Tor Browser'kupakua toka katika nakala mojawapo iliyo rasmi.

GetTor Bot