Tor Browser hutumia mtandao wa Tor kulinda faragha yako na kutojulikana. kutumia mtandao wa Tor kuna sifa kuu mbili:

  • Mtoa huduma wa mtandao wako, na yeyote anayeangalia mawasiliano yako ya ndani, hatoweza kufuatilia shughuli zako kwenye mtandao, ikijumuisha majina na anwani za tovuti unazotembelea.

  • waendeshaji wa tovuti na huduma unazotumia, na yeyote anayewaangalia,ataona mawasiliano yanatoka mtandao wa Tor badala ya anwani ya mtandao wako halisi, na hatajua wewe ni nani mpaka utakapojitambulisha.

Kwa kuongezea, Tor Browser imetengenezwa kuzuia tovuti kufanya “fingerprinting”au kukutambua kulingana na uundwaji wa kivinjari chako.

Moja kwa moja Tor Browser haitunzi kumbukumbu yoyote ya kuperuzi. Vidakuzi hufanya kazi kwa kipindi kimoja tu (mpaka Tor Browser inapotolewa au New identity inapoombwa).

NAMNA TOR HUFANYA KAZI

Tor ni mtandao usioonekana kwa kushikika uliofichwa unaokuruhusu kuboresha faragha yako na usalama katika mtandao. Tor hufanya kazi kwa kusafirisha taarifa zako katika seva tatu zisizo katika mpangilio (pia hufahamika kama relays) katika mtandao wa Tor. Relay ya mwisho katika circuit (“exit relay") kisha hutuma taarifa katika mtandao wa umma.

Jinsi Tor inavyofanya kazi

Picha hapo juu inaonyesha mtumiaji wa kivinjari katika tovuti mbalimbali badala ya Tor. Kompyuta ya kijani ya katikati inawakilisha relays kwenye mtandao wa Tor, wakati funguo tatu zinawakilisha matabaka ya usimbaji wa kila relay.