Unapounganishwa katika tovuti, sio tu waendeshaji wa tovuti husika wanakuwa na uwezo wa kuchukua taarifa zako kuhusiana na ulivyotembelea. Tovuti nyingi sasa hutumia huduma toka kwa watoa huduma wa nje mbalimbali, ikijumuisha mitandao ya kijamii "kama"vitufe, wadukuzi wa uchambuzi na nguzo za matangazo zote ambazo huunganisha shughuli zako toka tovuti mbalimbali.

Kutumia Tor mtandao huzuia wafuatiliaji kutambua eneo ulilopo na anwani yako ya IP, lakini bila hata ya hii taarifa wanauwezo wa kuunganisha maeneo tofauti ya shughuli zako pamoja. Kwa sababu hii, Tor Browser hujumuisha baadhi ya tabia za ziada ambazo zinakusaidia kudhibiti aina ya taarifa za kuwa katika utambulisho wako.

SEHEMY YA KUANDIKA URL

Tor Browser hukusanya uzoefu wako katika mtandao kuhusiana na mahusiano yako na tovuti katika sehemu ya URL. Hata kama utaunganisha katika tovuti mbili tofauti ambayo zinatumia watoa huduma wa nje wanaofanana katika shughulki za ufuatiliaji, Tor Browser italazimisha maudhui kuifadhiwa katika Tor Circuit mbili tofauti ili mfuatiliaji asijue kuwa mawasiliano yote yalitokea katika kivinjali chako.

Kwa upande mwingine, mawasiliano yote katika anwani moja ya tovuti yatakuwa yakifanywa katika Tor Circuit ileile, kumaanisha kuwa unaweza kuperuzi katika kurasa tofauti za tovuti moja katika window tofauti, bila kupoteza namna yoyote ya utendaji kazi.

Onyesha mchoro wa circuit chini ya machaguo ya taarifa za tovuti

Unaweza kuona mchoro wa circuit ambao Tor Browser inatumia katika kurasa iliyowazi katika menyu tovuti ya taarifa, katika sehemu ya URL.

Katika circuit,Guard au entry node ni node ya kwanza na huchaguliwa mojakwamoja bila mpangilio maalum na Tor. Lakini ni tofauti na nodes nyingine katika circuit. Ili kuepuka kuhakiki shambulio, Guard node hubadilika baada ya miezi 2-3, tofauti na nodes nyingine,ambayo hubadilika na kila kikoa kipya. kwa taarifa zaidi kuhusiana na Guards, fuatilia FAQ na Support Portal.

INGIA KATIKA PROGRAM YA TOR

Japokuwa Tor Browser imetengenezwa ili kuzuia kufahamika kabisa kwa mtumiaji katika tovuti, kunaweza kuwa na hali ambayo inamfanya mtumiaji kutumia Tor na tovuti ambazo zinahitaji jina la mmtumiaji, nenosiri au taarifa zingine za utambuzi.

Kama utaingia katika tovuti kwa kutumia kivinjari cha kawaida, pia utaonesha anwani yako ya IP na eneo ulilopo katika mchakato huo. Pia hii hutokea unapotuma barua pepe. Unapoingia katika mitandao yako ya kijamii au akaunti za barua pepe kwa kutumia Tor Browser inakuruhusu kuchagua aina gani ya taarifa za kuweka wazikatika tovuti unayoperuzi. Kuingia kwa kutumia Tor Browser pia inafaa kama tovuti unayoingia ipo salama katika mtandao wako.

Kama utaingia katika tovuti kwa kutumia Tor, kuna vitu mbalimbali vya kuzingatia:

  • Angalia kurasa Mawasiliano salama kwa taarifa muhimu za namna yakufanya mawasiliano salama unapoingia.
  • Tor Browser wakati wote hufanya mawasiliano yako kuonekana kama yanatokea sehemu tofauti ya dunia. Baadhi ya tovuti, kama vile benki au watoa huduma za barua pepe, wanaweza kuatafsiri hii kama kiashiria cha kudukuliwa kwa akaunti yako, na kukufungia. Njia pekee ya kusuluhisha hili ni kwa kufuata hatua zilizoshauriwa na tovuti kwa ajili ya kurudisha akaunti au kwa kuwasiliana na watoa huduma na uelezee hali ilivyo.

BADILI UTAMBULISHO NA SAKITI

New Identity na Circuit mpya ya Tor machaguo chini ya chaguo kuu

Machaguo ya sifa za Tor Broswer za “New Identity” na “New Tor Circuit kwa tovuti hii". Pia zinapatikana katika menyu kuu au menyu iliyofichwa (≡).

NEW IDENTITY

Machaguo haya yatafaa kama, unataka kuzuia shughuli za baadae za kivinjari kuunganishwa na kile ulichokuwa unafanya kabla. Kuichagua hii itafunga kurasa zote zilizo wazi, kufuta taarifa zote binafsi kama vile vidakuzi na historia ya kuperuzi, na kutumia Circuit mpya ya Tor kwa mawasiliano yote. Tor Brpwser itakuonya kuwa shughuli zoten na kupakua zitasitishwa, kwahiyo zingatia hili kabla huja bofya “New Identity”.

Kutumia chaguo hili, utahitajika kubofya'New Identity' katika mstari wa machaguo wa Tor Browser's toolbar.

TOR CIRCUIT MPYA KWA TOVUTI HII

Chaguo linaweza kutumika kama exit relay unayotumia haina uwezo wa kuunganisha katika tovuti unayohitaji, au haifungui vizuri. Kuichagua kutasababisha kurasa iliyo wazi kufunguliwa katika Tor Circuit mpya. Kurasa zingine zilizo wazi kutoka katika tovuti moja zitatumia circuit mpya pia pale zitakapo funguliwa tena. Machaguo haya hayatafuta taarifa zozote binafsi au kukata mawasiliano ya shughuli zako katika tovuti.

Pia unaweza pata haya machaguo katika circuit mpya, katika menyu ya taarifa za tovuti, katika sehemu ya URL.