Kama taarifa binafsi kama kuingiza nenosiri zikisafirishwa bila kusimbwa katika mtandao, iinaweza kiutambuliwa kwa urahisi na watu wasiohusika. Kama unaingia katika tovuti yoyote, yhakikisha kwamba tovuti ina usimbwaji wa HTTPS , ambao hulindwa na wadukuzi wa aina hii.Unaweza kuhakiki hii katika sehemu ya URL: kama mawasiliano yako yamesimbwa, anwani itaanza na “https://”, badala ya“http://”.

HTTPS-Mfumo pekee katika Tor Browser

Mfumo pekee wa HTTPS-hulazimisha mawasiliano yote katika tovuti kuwa salama na kuwa yaloiyosimbwa huitwa HTTPS. Tovuti nyingi sasa hutumia HTTPS; baadhi hutumia zote HTTP na HTTPS. Kuruhusu mfumo huu katika mawasiliano yako ya tovuti yatawezeshwa kutumia HTTPS na yatakuwa salama.

HTTPS-imetengenezwa kwa ajili ya Tor Browser

Baadhi ya tovuti hukubali HTTP pekee na mawasiliano hayawezi kuboreshwa. Kamatoleo la HTTPS ya tovuti inapatikana, utaona kurasa ya “mawasiliano salama hayapo”:

Hakuna mawasiliano salama kama tovuti ni ya HTTP

Kama utabofya 'endelea katika tovuti ya HTTP ' umekubali hatari na utatembeleatovuti ya toleo la HTTP. Mfumo wa HTTPS-Only utazimwa kwa muda katika tovuti.

Bofya kitufe cha 'Go Back' kama unataka kukwepa mawasiliano yasiyo simbwa.

Mchoro ufuatao unaonyesha taarifa zipi zinaonekana kwa wasikilizaji wa siri ukitumia au usipotumia usimbwaji wa Tor Browser na HTTPS:

  • Bonyeza kitufe cha “Tor” kuona data gani inaonekana kwa waangalizi wakati unatumia Tor. Kitufe kitakua cha kijani kuonesha kuwa Tor ipo inatumika.
  • Bofya kifufe cha “HTTPS” kuona data zipi zinaonekana kwa wafuatiliaji unapokuwa unatumia HTTPS. Kitufe kitabadilika na kuwa kijani kuonesha kuwa kuna HTTPS.
  • Vitufe vyote vikiwa vya kijani, unaona data zinazoonekana kwa wafuatiliaji unapokuwa unatumia vifaa vyote.
  • Vitufe vyote vikiwa vya kijivu, unaona data zinazoonekana kwa wafuatiliaji wakati ambao hutumii kifaa chochote.



DATA ZA MUHIMU ZA KUONEKANA
site.com
Tovuti iliyokuwa ikitembelewa.
Mtumiaji / pw
Jina la mtumiaji na nenosiri vilivyotumika kwa ajili ya uhakiki.
data
Data zilizokuwa zikisambazwa.
Eneo
Eneo la mtandao iliyopo kompyuta iliyotumika kutembelea tovuti (anwani ya IP ya wazi).
Tor
Kama Tor ilikuwa ikitumika au haikutumika.