Tor Browser ya Android

Tor Browser ya Android ni programu pekee iliyo rasmi kwa ajili ya vifaa vya mkononi inayowezeshwa na kutengenezwa na Tor Project. Ni kama Tor Browser ya kompyuta, lakini ni kwa vifaa vya android vya mkononi. Baadhi ya sifa za kipekee za Tor Browser ya Android inahusisha :kupunguza kufuatilia tovuti, kutambua ufuatiliwaji, kukabili utambuzi wa kipekee wa kivinjari, na kukwepa udhibiti.

KUPAKUA NA USAKINISHAJI

Hapo inakaa Tor Browser ya android na Tor Browser ya Android (alpha). Watumiaji wasio wataalamu wanatakiwa kupata Tor Browser ya android, sababu hii inautulivu na ina dosari chache sana. Tor Browse ya Android inapatikana katika Play Store, F-Droid na tovuti ya Tor Project. Ni hatari sana kupakua Tor Browser nje ya sehemu hizi tatu.

Google Play

Unaweza kusakinisha Tor Browser ya Android kutoka katika Google Play Store.

F-Droid

The Guardian Project hutoa Tor Browser ya Android katika hifadhi zao za F-Droid. Kama utapenda kusakinisha programu kutoka katika F-Droid, tafadhali fuata hatua zifuatazo:

 1. Sakinisha program ya F-Droid app katika kifaa chako cha Android kutoka the F-Droid website.

 2. Baada ya kusakinisha F-Droid, fungua programu.

3.Kona ya kulia chini, Fungua "Settings".

 1. Chunu ya sehemu ya "My Apps", fungua sehemu ya kuhifadhi data.

 2. Geuza"Guardian Project Official Releases" kama iliyo wezeshwa.

 3. Sasa F-Droid hupakua orodha ya programu kutoka katika hazina ya Guardian Project(Zingatia: hii inaweza chukua dakika kadhaa).

 4. Bofya kitufe cha kurudi katika kona ya kushoto juu.

 5. Fungua"Latest" katika kona ya kushoto chini.

 6. Fungua ukurasa wa kutafuta kwa kubofya sehemu ya kukuza uoande wa kulia chini.

 7. Tafuta "Tor Browser ya Android".

 8. Fungua taarifa za matokeo kwa "Tor Project" kisha sakinisha.

Tovuti ya Mradi wa Tor

Pia unaweza kuipatat Tor Browser ya Android kwa kupakua na kusakinisha apk kutoka katika Tor Project website.

KUTUMIA TOR BROWSER KWA ANDROID KWA MARA YA KWANZA

Unapotumia Tor Browser kwa mara ya kwanza, yutapata machaguo ya kuunganisha mojakwamoja katika mtandao wa Tor, au kusanidi Tor Browser kwa ajili ya mawasiliano yako katika alama ya mpangilio.

Unganisha

Jiunganishe katika Tor Browser ya Android

Mara nyingi, kuchagua"Connect" itakuruhusu kuunganisha katika mtandao wa Tor bila usanidi wa ziada. Pale tu inapoguswa. kutatokea kubadilishwa kwa sentensi chini ya skrini, ikionesha kuendelea kwa mawasiliano ya Tor. Kama upo katika mawasiliano yenye kasi ya haraka, lakini ujumbe huu unaonekana kukwama mahali, angalia kurasa ya Troubleshooting kupata msaada wa kutatua tatizo hilo.

Sanidi

Sanidi Tor Browser kwa ajili ya Android

Kama unajua kuwa mawasiliano yako yamedhibitiwa, unatakiwa kuchagua kitufe cha mpangilio. Tor Browser itakupeleka katika machaguo kadhaa ya kusanidi. Skrini ya kwanza itakupa taarifa ya hali ya mtandao wa Tor na kukupa chaguo la kusanidi Bridge ('Config Bridge'). Kama unajua mtandao wako umedhibitiwa au umejaribu na umeshindwa kujiunga katika mtandao wa Tor na hakuna suluhisho lingine limepatikana, bofya katika 'Config Bridge'. Utapelekwa katika Kukwepa udhibiti kurasa ya kusanidi pluggable transport.

KUKWEPA UDHIBITI

Relays za Bridge ni relays za Tor ambazo hazitaorodheshwa katika umma ya sakara ya Tor. Bridges hufaa kwa watumiaji wa Tor bila sheria, na kwa watu wanaohitaji tabaka za ziada la ulinzi sababu wanahofia mtu anaweza kuwatambua kuwa wanawasiliana kutumia anwani ya IP ya Tor relay.

Kutumia pluggable transport, bofya katika alama ya mpangilio unapoanza Tor Browser kwa mara ya kwanza. Skrini ya kwanza inaelezea hali ya mtandao wae Tor. Bofya katika'Config Bridge' ili kusanidi bridge.

Mtandao uliodhibitiwa katika Tor Browser ya Android

Skrini inayofuata itakupa chaguo la kutumia bridge iliyoundwa katika mfumo au bridge ya kutengeneza. Kwa kutumia chaguo la "Use a Bridge"utakuwa na machaguo matatu: "obfs4", "meek-azure", and "snowflake".

Chagua bridge katika Tor Browser ya Android

Chagua a bridge katika Tor Browser ya Android

Kama utachagua chaguo la "Provide a nBridge I know",kisha utahitajika kuweka bridge address.

Weja bridge katiuka Tor Browser ya Android

Weka anwani ya bridge katika Tor Browser ya Android

KUSIMAMIA VITAMBULISHI

New Identity

New Identity katika Tor Browser ya Android

Wakati Tor Browserinafanya kazi, utapata taarifa katika kifaa chako baada ya kufungua taarifa ya "NEW IDENTITY". Kubofya katika kitufe hicho kitakulketea new identity. Kinyume na Tor Browser ya kompyuta, kitufe cha "NEW IDENTITY"katika Tor Browser ya Android haizuii shughuli za kivinjali chako kinachofuata kuunganishwa na kile ulichokuwa unafanya kabla. Kwa kuchahua hivyo itabadilisha Tor circuit yako.

MPANGILIO WA ULINZI

Mpangilio wa ulinzi katika Tor Browser ya Android

Mpangilio wa ulinziondoa baadhi ya tabia za tovuti ambazo zinaweza kusumbua ulinzi na kutofahamika. Tor Browser ya Android hutoa hatua zilezile tatu za ulinzi ambazo zinapatikana katika kompyuta. Unaweza kuboresha kiwango cha usalama kwa kufauata hatua zifuatazo:

 • Gusa kitufe cha vidoti 3 vya wima katika sehemu ya URL.
 • Shusha chini na gusa katika "Security Settings".
 • Sasa unaweza kuchagua chaguo la i.e. Kiwango, Salama zaidi or Salama sana.

KUSASISHA

Tor Browser ni lazima isasishwe wakati wote. Kama unaendelea kutumia toleo lililopitwa na wakati la programu, unaweza kuwa katika hatari ya kupata tatizo kubwa la kiusalama ambazo zitasumbua faragha na kutojulikana kwako. Unaweza kusasisha Tor Kivinjari kiautomatiki au kiumongozo.

Kusasisha Tor Kivinjari kwa Android kiautomatiki

Njia hii huamini kwamba inaweza ukawa na Google Play or F-Droid imesanidiwa katika kifaa chako cha mkononi.

Google Play

Sanikisha Tor Browser ya Android katika Google Play

 • Open the Google Play Store app.
 • At the top right, tap the profile icon.
 • Tap on 'Manage apps and devices'.
 • Tap on the 'Manage' tab.
 • Tap on 'Updates available'
 • Tap on Tor Browser for Android from the list of apps that need to be updated.
 • Tap on 'Update'.
F-Droid

Sakinisha Tor Browser ya Android katika F-Droid

Bofya katika "Settings", kisha nenda katika "Manage installed apps". Katika skrini inayofuata, chagua Tor Browser kisha bofya kitufe cha "Update".

Sanikisha Tor Browser ya Android kawaida

Tembelea tovuti ya Tor Project pakua nakala ya toleo jipya la Tor Browser, kishasakinisha kama ilivyokuwa mwanzo. Mara nyingi, toleo hili jipya la Tor Browser hujisanikisha katika toleo la zamani, hivyo huboresha kivinjari. Kama kufanya hivi itashindwa kusasisha kivinjari, unaweza kuhitajika kuitoa Tor Browserkabla ya kusakinisha. Tor Browser ikiwa imefungwa, toa katika mfumo wako kwa kutumia mpangilio wa programu ya kifaa chako. Kulingana na aina ya kifaa chako, nenda katika Settings > Apps, kisha chagua Tor Browser kisha bofya kitufe cha "Uninstall" . Baada ya hapo, pakua toleo jipya la Tor Browser kisha sakinisha.

KUONDOA

Tor Browser ya Android inaweza kutolewa mojakwamoja kutoka katika F-Droid, Google Play au kutoka katika mpangilio wa programu wa kifaa chako cha mkononi.

Google Play

Sanidisha Tor Browser ya Android katika Google Play

 • Open the Google Play Store app.
 • At the top right, tap the profile icon.
 • Tap on 'Manage apps and devices'.
 • Tap on the 'Manage' tab.
 • Tap on Tor Browser for Android from the list of apps installed on your device.
 • Tap on 'Uninstall'.

F-Droid

Sanidisha Tor Browser ya Android katika F-Droid

Bofya katika "Settings", kisha nenda katika "Manage installed apps". Katika skrini ifuatayo, chagua Tor Browser na kisha bofya katika kitufe cha "{uninstall".

Mipangilio ya programu kwenye kifaa cha Simu

Sanidisha Tor Browser ya Android kutumia mpangilio wa program ya kifaa

Kulingana na aina ya kifaa chako, Nenda katika mpangilio > Apps, kisha chagua Tor Browser bofya katika klitufe cha "Uninstall".

TROUBLESHOOTING

Angalia dosari za Tor

Angalia dosari za Tor katika Tor Browser ya Android

Kungalia dosari katika Tor yako:

 1. Anza kutumia Tor Browser ya Android na bofya 'Connect'.
 2. Wakati wa shughuli ya kuchakata data, pangusa kulia kwenda kushoto kuona kama kuna dosari zozotes. (Zingatia: Mojakwamoja, huwezi kupiga picha skrini yadosari za Tor katika Tor Browser ya Android. #41195)

If you want to share the error logs with us, you can take a screenshot. By default, screenshots are disabled in Tor Browser, but you can enable them. To do this, please follow these steps:

 • Tap the menu button (at the bottom of the screen on the right side next to the address bar, three dots vertically).
 • Then tap 'Settings'.
 • Go to 'Advanced' section.
 • Toggle 'Allow screenshots'.

Kusuluhisha baadhi ya matatizo ya kawaida tafadhali zingatia katikaSupport Portal entry.

MASUALA YANAYOJULIKANA

Wakati mwingine, kuna baadhi ya vitu havipo katika Tor Browser ya Android, lakini kwa kawaida vipo katika Tor Browser ya kompyuta.

 • Huwezi kuiona Tor circuit. #41234
 • Tor Browser ya Android haiunganishi inapokuwa katika SD Card. #31814
 • Huwezi kupiga picha skrini ya kifaa chako unapotumia Tor Browser ya Android. #27987
 • Huwezi kufungua anwani za huduma zilizofichwa ambazo zinamuhitaji Client Authorization #31672

Zaidi kuhusiana na Tor ya vifaa vya mkononi

Orfox

Orfox kwa mara ya kwanza ilitolewa mwaka 2015 na mradi wa The Guardian, kwa lengo la kuwapatia watumiaji wa android njia ya kuperuzi mtandaoni kwa kutumia Tor. Kwa maiaka mitatu iliyofuata ,Orfox iliboreshwa na kuwa namna maarufu ya watu kuperuzi kwa faragha zaidi kuliko kivinjari kingine vya kawaida, na Orfox ikawa muhimu katika kusaidia watu kukwepa udhibiti wa mtandao na kuzipata tovuti zilizozuiliwa na vyanzo muhimu. Mwaka 2019, Orfox iliisha baada ya Tor Browser rasmi ya Android kuanzishwa.

Orbot

Orbot ni programu huru ya proxy ambayo inawezesha programu zingine kutumia mtandao wa Tor. Orbot hutumia Tor kusimba usafirishaji wa data zako mtandaoni. Kisha unaweza kutumia pamoja na programu zingine zilizosanidiwa katika kifaa chako cha mkononi ili kukwepa udhibiti na kulinda ufuatiliwaji. Orbot inaweza kupakuliwa na kusakinishwa kutoka katika Google Play. Angalia our Support portal kama unahitaji vyote Tor Browser ya Android naOrbot kimoja wapo.

Tor Kivinjari kwa iOS

Hakuna Tor Kivinjari kwa iOS. Tunashauri proramu ya iOS inayoitwa Onion Browser, ambayo inapatikana bure kwa uwazi, kutumika kusafirisha, na imetengenezwa na mtu ambaye anafanya kazi kwa ukaribu na Tor Project. Hatahivyo, Apple huitaji kivinjari katika iOS kutumia kitu kinaitwa Webkit, ambayo huzuia Onion Browser kuwa na ulinzi wa faragha kama uliopo katika Tor Browser.

Jifunze zaidi kuhusu Onion Kivinjari. Pakua Onion Kivinjari kwenye App Store.

Tor Kivinjari kwa Simu ya Windows

Kwa sasa hakuna njia inayokuwezesha kutumia Tor katika simu window za zamani lakini kwa simu za toleo jipya zenye mfumo mpya wa microsoft fuata hatua kupitia Tor Browser on Android zinaweza kufauatwa.